top of page

Accountability 

Register

ACCOUNTABILITY REGISTER

REJISTA YA WAJIBU INAYOONESHA MAPENDEKEZO YA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI YATOKANAYO NA UKAGUZI WA MASHIRIKA YA UMMA KWA KIPINDI CHA MWAKA 2013/14 HADI MWAKA 2015/16 Utangulizi WAJIBU – Taasisi ya Uwajibikaji wa Umma katika kutekeleza malengo yake ya kukuza uwajibikaji na utawala bora hapa nchini, imeandaa Rejista ya Uwajibikaji yenye lengo la kurekodi na kufuatilia utekelezaji wa mapendekezo yote muhimu yaliyo pendekezwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) katika ripoti zake za ukaguzi wa Mashirika ya Umma katika kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2013/14 hadi 2015/16. Madhumuni makuu ya rejista hii ni kuyafanya mapendekezo ya CAG kuwa hai kwa kipindi kirefu zaidi kuliko ilivyo sasa na hivyo kuongeza uwezekano wa ufuatiliaji na utekelezaji wa mapendekezo hayo. Vilevile, kwa kila pendekezo, WAJIBU imefanya uchambuzi wa umuhimu wa pendekezo lililotolewa, faida za utekelezaji wake, namna utekelezaji unavyoweza kufanywa, mamlaka inayohusika katika utekelezaji huo na hali ya utekelezaji wa pendekezo hilo. Rejista hii inalenga katika kuhimiza utekelezaji wa mapendekezo ya CAG ambao utapelekea kuimarika na kukuza zaidi uwajibikaji na utawala bora hapa nchini hivyo kuongeza kasi ya maendeleo ya nchi.

bottom of page